Bunge la senet limepitisha mswada utakaopelekea vijana wanaomaliza shule za
upili nchini kujiunga na huduma ya vijana NYS kabla ya
kujiunga na vyuo vikuu au vyuo vingine vya mafunzo.
Hatua hiyo imechukuliwa ili kuwezesha
vijana kupata mafunzo ya taaluma tofauti na kupalilia uzalendo kabla ya
kujiunga na masomo ya vyuo vikuu au shughuli zozote baada ya kumaliza shule za
upili.
Haya ni marudio ya hali
ilivyokuwa hadi 1989 ambapo walioteuliwa
kujiunga na vyuo vikuu kwanza walipata mafunzo ya miezi mitatu katika NYS.
Seneti ilipitisha kwa kauli
moja hoja hiyo iliyowasilishwa na seneta maalum, Beatrice Elachi aliyetaka wanaomaliza masomo ya shule za sekondari
wasaidiwe kujiunga na NYS ili wapate mafunzo muhimu.
Katika hoja yake, Elachi ambaye pia ni kiranja wa walio
wengi katika seneti, anataka wanaohitimu baada ya kupata mafunzo kutoka NYS,
wapatiwe nafasi ya kwanza ya ajira katika serikali za kaunti na serikali kuu.
Maseneta wamesema kufanya hivyo
kutawasaidia vijana wa nchi hii waafikie haki zao za kiuchumi na kijamii.
No comments:
Post a Comment